Teachings


NAMNA YA KUGUNDUA DALILI NA VYANZO VYA LAANA 
The Oasis of Healing Ministries
IMEANDIKWA Na Pastor K. Ntepa
(0713 212440 AU 0755029602)

Karatasi hii (questionnaire) ina maswali na vipengele mbalimbali ambavyo vitakusaidia kugundua dalili za laana na vyanzo vya laana. Naomba uweke tiki () katika sehemu ile ambayo unaona kuwa ni dalili au chanzo cha laana ambacho unacho. Kugundua tatizo ni nusu ya suluhisho. Sehemu ambayo unaona haikuhusu acha wazi. Vifungo na laana vinaletwa na mapepo. Ukihitaji maombi ya kufunguliwa kutoka katika laana na vifungo unaweza kuja katika kanisa la The Oasis of Healing Ministries lililoko nyuma ya jengo refu la Ubungo Plaza karibu na kanisa la Anglikana na shule ya msingi Ubungo National Housing. Siku ya maombezi ya mtu mmoja mmoja ni siku ya Jumamosi saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 na Jumatano saa 8:00 hadi saa 12:00 jioni. Siku za ibada ni Alhamisi saa 10:00-12:30 na Jumapili saa 2:00 hadi saa 4:00 ni ibada ya Kiingereza na saa 4:00 hadi 7:30 alasiri ni ibada ya Kiswahili na ibada ya jioni ni saa 10:00 hadi 12:30. 

        1.   ASILI YA WAZAZI /MABABU
Kuna laana ambazo zina mizizi kwa wazazi au babu zako. Unaweza kubarikiwa au kulaaniwa kupitia matendo na mikataba ya wazazi (Kutoka 20:4-5; Mithali 20:7).
     (a)    Je wazazi wako ni watu wa namna gani? Watu wa dini sana……………….. Washirikina?………………… Waganga wa kienyeji?……………………………. Wenye kuabudu mizimu?…………………………………………………………..
     (b)    Je babu kwa upande  wa baba ni mtu wa namna gani/walikuwa mtu wa namna gani?……………… Mtu wa dini sana?……………. Mshirikina?…………………….. Mganga wa kienyeji? ………………… mwenye kuabudu mizimu?  

        2.   MAGONJWA NA MATATIZO YALIYO KATIKA FAMILIA YAKO:

Je ni matatizo gani kati ya haya yapo kwenye familia (Baba, mama, dada, kaka, binamu mjomba, shangazi n.k)?
       (a)    Kansa………………………..  (b) Ugonjwa wa moyo…………………….
(c) B.P. (Shinikizo la damu)………………(d) Kuachana katika ndoa (divorce)?
      (e)    Mimba kabla ya ndoa?………………………………………………
       (f)     Ugonjwa wa kisukari  (diabetes) (g) Kujiua…………………………
(h) Kuchanganyikiwa?……………………. (i) Sickle cell?………………….
       (j)       Vifo visivyo vya kawaida katika familia? ……………………………………
       (k)     Ajali za mara kwa mara?……………………………………
        (l)       Kuoa wake wengi (polygamy)?……………………………..
       (m)   Mimba kuharibika?………………………………….
        (n)     Ulcers (vidonda vya tumbo)?………………………………..
        (o)     Pumu?……………..  (p) Je ni ugonjwa/magonjwa ipi au yapi unakusumbua/ yanakusumbua mpaka sasa? ………………………………………………………….


        3.    JINA
Je una jina la kurithi/kupewa lenye maana mbaya, ukiri mbaya au linalobeba athari fulani katika maisha yako?

      4.      Vifungo vingine
 Taja vifungo vingine hapa chini vinavyokusumbua:
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

      5.    Dalili za kuwa na laana
Je unazo dalili zifuatazo za laana katika maisha yako?
      (a)    Magonjwa ya akili kuharibikiwa kiakili au kuhisi (kwa mfano kuchanganyikiwa au kupata kichaa?………………….
      (b)    Magonjwa yanayorudia rudia au sugu na hasa kama ni ya kurithi au bila kugundulika wazi na hospitali (magonjwa ya mifupa (arthritis au rheumatism), shinikizo la damu, kisukari, kansa………………………………………………….
      (c)    Utasa, mimba kutoka au kuharibika mara kwa mara au matatizo yanayofanana na hayo ya wanawake. Kwa mfano kusikia maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi ………………………. Taja ………………………….
      (d)   Siku za hedhi kubadilika badilika, uvimbe katika tumbo la uzazi
      (e)    Damu ya hedhi kutoka mfululizo ………………………………………………….
       (f)     Kuharibika kwa ndoa au kutengwa kwa familia kwa ujumla………………………
       (g)    Hali ya talaka au kuachana katika familia …………………………………………
       (h)    Magomvi katika ndoa, magomvi kati ya wanandugu …………………………….
        (i)      Matatizo sugu ya kifedha kama upungufu wa fedha  unaoendelea na hasa mahali  ambapo mapato yanaonekana kuwa yanatosha?……………………………..
        (j)      Hali ya kuwa na madeni mara kwa mara, kufilisika, n.k.
        (k)    Chochote unachokifanya hakifanikiwi; kutawaliwa na hali kushindwa …………..
        (l)      Kuwa mkia kila wakati na kuwa hali ya chini …………………………………….
       (m)  Hali ya kuwa nyuma (backwardness) na kutofikiwa kwa malengo katika maisha
        (n)    Kufanya kazi kwa kutumia nguvu sana bila matunda…………………………….
        (o)    Kudhalilishwa na kupata aibu ………………………………………………..
        (p)    Kuachishwa kazi mara kwa mara bila sababu za msingi, kutokupata kazi ………..
        (q)    Kupoteza fedha kwa njia za ajabu au bila sababu ………………………………
         (r)     Kupata hasara mara kwa mara katika biashara na miradi ………………………
         (s)     Kukosa kibali, radhi au upendeleo au hali ya kukataliwa na watu
        (t)     Kuporwa au kutekwa nyara ……………………………………….
        (u)    Kutokuolewa au kutokuoa au kukataliwa na wachumba ………………………
        (v)    Kuonewa na maadui zako na wapinzani wako bila kipingamizi chochote ……….
        (w)  Kufanyiwa vibaya na kunajisiwa na watu wengine ………………………………
         (x)    Roho ya kutangatanga au kutokuwa na hali ya kutulia, utoro (vagabond). Kuwa na hali ya kuhamahama kutoka kazi moja hadi nyingine, mji mmoja hadi mwingine, kanisa moja hadi jingine.
        (y)    Huzuni, kukandamizwa na kukata tamaa
        (z)    Kujirudiarudia kwa mabaya katika maisha yako bila uwezo wa kuzuia…………...

        6.    Dalili zingine za laana

        (aa)  Kuzidi kuwa dhaifu au kupungua nguvu kiuchumi
        (bb)                       Hali ya kuwa na vizingiti (setbacks), vikwazo, maendeleo ya kiuchumi kuwa katika mwendo wa pole pole, au kuchelewa kwa mafanikio yako kila wakati.
        (cc)  Kuwa na mambo magumu au mabaya yanayofanana kati ya wanafamilia ……
        (dd)                      Kuwa na hali ya kupata ajali za mara kwa mara?…………………………
        (ee)    Kuwa na historia ya kujiua au vifo visivyo vya asili katika familia, ndugu kufa kabla ya wakati?………………
        (ff)  Kuwa na vifungo vya pepo mahaba yaani kuota mara kwa mara unajamiiana na mtu   ambaye siyo mume au mke wako. Pepo mahaba wanaleta vifungo vya umaskini na laana ya kutokufanikiwa katika mambo unayoyafanya.

      7.       Vyanzo au milango ya kupata laana
Je katika vyanzo hivi vya laana ni kipi uliwahi kuwa nacho au unacho mpaka sasa?
            (a)                 Kuwa na historia katika familia ya kuabudu miungu mengine, miungu ya uongo,
            (b)                 Maovu ya wababa kwa mfano, kushiriki kwenye ushirikina kwa wewe mwenyewe au mojawapo wa baba au babu………………………..
            (c)                 Kutokuheshimu wazazi au kuwa na mtazamo mbaya juu ya wazazi?……………………….
            (d)                Zinaa iliyo kinyume na sheria na isiyo ya asili. Zinaa na ndugu wa karibu kama dada, kaka, binamu, (incest) ulawiti, kulala na mnyama [kuku, mbuzi n.k]?
          (e)                 Kuwaonea wanyonge wasio na msaada? Kwa mfano kutoa mimba, ?……………………
          (f)                  Kutegemea mkono wa nyama au wanadamu wanadamu?……………………
          (g)                 Kuiba au uongo wa makusudi (stealing or forgery)…………………….
          (h)                 Kutokutoa zaka kwa uaminifu au kuwa mchoyo kwa Mungu…………………
           (i)                   Maneno mabaya yaliyotamkwa na watu wenye mamlaka ya kindugu kwa mfano wazazi, mume, walimu au wachungaji?………………………
           (j)                   Kujilaani mwenyewe, laana ambazo wewe mwenyewe umejitamkia mabaya, kifo, ukiri mbaya wa kushindwa na kutokufanikiwa …………………………
          (k) Maneno yanayotamkwa na watu wanaomwakilisha shetani kwa mfano waganga wa kienyeji ili kukuloga, wachawi kukutabiria mabaya kwa mfano ajali, kifo?……………….
          (l)   Watu wengine kufanaya maombi ya kimwili au maombi yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu juu ya maisha yako na matamshi yaliyosemwa kwa nia mbaya na masengenyo dhidi yako yanayokutabiria mabaya?………………
          (m)  Maagano yasiyo ya kimaandishi (yaani maagano ya kutamka), kuunganika kwa njia ya agano na watu walio na umoja na nguvu za mabaya na za kigeni kwa Mungu kama vile waganga wa shetani, mawakala wa shetani.
          (n) Kushiriki katika mambo ya uchawi, mambo ya siri ya giza (occult) na dini za uongo.
          (o)Kuleta vitu au vyombo vilivyolaaniwa katika nyumba au ofisi kwa mfano vinyago, zawadi ambazo umepewa kwa nia mbaya na zilizonuiziwa nguvu za giza.
          (p)Mababu kukubali laana zije yao na juu ya uzao wao yaani watoto na wajukuu.
          (q)Kufanya mila na desturi za kipepo
          (r)Majina ya kurithi au yenye maana na ukiri mbaya
           (s)               Kwenda kinyume na haki maalum za shetani au mapepo katika maeneo fulani
          (t)                  Kukaa katika nyumba au nchi yenye laana
          (u)                 Kuvunja mkataba maalum wa kujitoa au kujiweka wakfu kwa shetani au mapepo
          (v)                 Kuwalaani, kuwatendea au kuwasema vibaya Wayahudi au taifa la Israeli.
          (w)               Kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu au uvivu
           (x)                 Kushindwa kuwasaidia maskini
           (y)                 Kutokumweshimu Mungu katika maisha yako
           (z)                 Kulaaniwa na wazazi- kutamkiwa mabaya kwamba hutafanikiwa, wewe siyo chochote, afadhali ungekuwa mvulana au msichana, wewe ni mpumbavu

     8.    Njia zingine zinazoweza kuleta laana

           (aa)               Kuwa na alama za kujikata (marks) katika mwili au kunyoa kwa ajili ya wafu.
           (bb)             Kutokuwatendea wengine kwa jinsi isio haki au kunyanganya haki ya wengine.
           (cc)              Kupata mali kwa jinsi isio haki
           (dd)            Kurudisha mabaya baada ya wewe kutendewa mema.
           (ee)              Kumwaga damu isiyo na hatia (shedding innocent blood)
            (ff)               Kufuata mambo ya kuagua kwa kutumia nyota
            (gg)             Kutoa sadaka za wanadamu au kafara
            (hh)             Kupata fedha kwa njia ya kuwauwa watu wasio na hatia

       9.    Dalili za Laana katika ndoto

 Je katika ndoto zako una dalili zifuatazo ambazo zinaweza kuashiria laana?
       (a)    Kupigana na watu usiowajua katika ndoto ambao wanakushinda
       (b)   Kuchelewa kila wakati kwa ajili ya mtihani au kazi maalum
       (c)    Kujiona uko katika shimo, gereza
       (d)   Kila wakati kuwasiliana na wafu
       (e)    Kuonewa au kuteswa katika ndoto
       (f)    Kuibiwa vitu vya thamani au fedha katika ndoto
       (g)   Kuanguka kutoka mahali pa juu kwenda chini.
       (h)   Kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye si mume au mke wako.
        (i)     Kuwa na ndoto za vitisho, kusema kila wakati katika ndoto (somnaloquist) au kutembea ukiwa katika ndoto (somnambulism). 

 
VITABU VILIVYO ANDIKWA NA WACHUNGAJI PROSPER NTEPA NA DEBORAH NTEPA
Vitabu vya Mtume Prosper Ntepa
       1.   Dalili 60 za Kuwa na Vifungo vya Pepo Wachafu (Sh 3500/)
       2.   Jinsi Ya Kujiandaa Kuoa na Kuolewa (Sh 5000/).
       3.   Siri Ya Kutunza Uponyaji Wako (Sh 6000/)
4.   30 Reasons Why You Can Be Healed of AIDS (vol. 1) (Sh 6000/).
       5.   Working with Diligence: A Pillar to Prosperity (Sh 4000/)
6.   Angels of Prosperity (Sh 6000/)
7.   Renewing Your Mind for Prosperity (4000/).
       8.   Sifa Saba za Cream (Sh 3000/)
        9.   Nguvu ya Shauku Kubwa: Aina 30 za Shauku (Sh 2500/)
       10.  Nguvu ya Shauku Kubwa katika Kupokea Uponyaji (Sh 2500/)
       11.   Je Mtu Anaweza Kuokoka Akiwa Duniani: Sababu 29 Kwa Nini Mtu Anaweza Kuokoka Akiwa Duniani (Sh 1500/)
       12.  Tofauti ya Kifo cha Mwenye Haki na Asiye Haki (Sh 1500/)
       13.  Vyanzo Saba vya Dawa ya Mungu: Jinsi ya Kupokea Uponyaji Wako (Sh 6000/)
       14.  Funguo Nne za Kupata Hakika ya Wokovu (Sh 2500/)
       15.  Jihadhari na Roho ya Uwastani (Sh 3000/)
       16.  Siri 10 za Kutembea Katika Upako: Faida 13 za Upako (Sh 3500/)
       17.  Mahitaji Makuu Matano ya Mume na Mke Katika Ndoa (Sh 7000/)
       18.  Ahadi, ukiri na maombi kwa ajiri ya Uponyaji na Afya
       19.  Tofauti ya kifo cha mwenye haki na Asiye na haki
       20.  Zaidi ya watu 35 waponywa ukimwi
       21.  Dalili 30 za baraka
       22.  Funguo saba za kuishi maisha marefu
       23.  Funguo saba za kukusaidia kujifunza kutoa unabii
       24.  Dawa ya Mungu kwa Ajiri ya Magonjwa

Vitabu Vya Mchungaji Deborah Ntepa (Kwa Kiswahili na Kiingereza)

         1.         Usikate Tamaa: Muujiza Wako Uko Njiani (3000/)
         2.         Utasa Unaponyeka (1500/)
         3.         Unaweza Kumsikia Mungu (3000/)
          4.         Jinsi ya Kupata Kibali (3000/)
          5.         Uponyaji wa Moyo ulioumizwa (3000/)
          6.         Vijue Vyanzo vya Magonjwa (3000/)
          7.         Jinsi ya Kujiandaa Kuolewa (3000/)
          8.         Nguvu ya Majina (3000/)
          9.         Jinsi ya Kuboresha Ndoa (3000/)
          10.     The Healing of the Broken Heart (3000/)
          11.     Do Not Give Up: Your Miracle is on Way (3000/)
          12.     How to Find God’s Favour (3000/)

1 comment:

  1. GREAT DADDY. I AM BEING BLESSED BY YOUR TEACHINGS. MAY MY GOD INCREASE YOU ORE AND MORE IN JESUS NAME.

    ReplyDelete